Local Bulletins

Mikakati ya kuhakikisha Amani na usalama wakati wa uchaguzi imewekwa. – Waziri Matiangi.

Waziri Wa Usalama Wa Ndani Fred Matiangi.
Picha; Hisani

Na Isaac Waihenya

Waziri wa Usalama nchini Daktari Fred Matiangi amewahakikishia washirika wa maendeleo hapa Nchini kuwa mikakati ya kuhakikisha Amani na usalama wakati wa uchaguzi imewekwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Matiangi amesema kuwa mipango ya kuhakikisha usalama wakati wa kampeni za uchaguzi, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi imewekwa na maeneo ambayo yanakisiwa kuwa yatakumbwa na ghasia kuatibitibiwa.

Aidha Matiangi amesema kuwa maafisa zaidi wa usalama wamepewa mafunzo ili kushika doria katika kipindi hicho huku tume ya Uiano na Utengamano nchini NCIC ikizidisha juhudi za kukabiliana na uchochezi.

Subscribe to eNewsletter