KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Mgombea wa kiti cha MCA wadi ya North Horr Tura Ruru Elema amekihifadhi kiti chake. Ruru ambaye amewania kwa tiketi ya chama cha KANU ameshinda kwa kupata kura 2978. Adano Salesa Galgallo wa Jubilee anamfuata Kwa kujizolea kura 2826. Isacko Budha wa UPIA amepata kura 588.
Afisa wa kituo cha kujumuisha kura eneo bunge la North Horr Franklin Chebii pia amemtangaza Mamo Huqa Galgallo kuwa mshindi wa kiti cha uwakilishi wadi Turbi. Huqa wa chama cha Jubilee amepata kura 2,379 na kumbwaga aliyekuwa MCA eneo hilo Guyo Duba Yaro wa Upia aliyepata kura 1924. Lohho Abduba amepata kura 69.
Boru Adano wa chama cha Upia ndiye MCA mteule wa wadi ya Dukana. Adano ametangazwa mshindi kwa kuzoa kura 2876 naye Bonaya Katello Sarboba wa Jubilee akimfuata kwa kura 2836. Umuro Mamo Liban amepata kura 72.
MCA wa Maikona Buke Diba amefaulu kukitetea kiti chake kwa kuibuka mshindi. Buke ambaye amewania kwa tiketi ya chama cha Upia ameibuka mshindi na kuwapiku Diba Kone Galgalo wa chama cha Jubilee ambaye amepata kura 2,404.
Wario Bulle wa chama cha DAP-K amepata kura 1,161. Wadi ya Maikona ina wapiga kura 9,865. James Haile Korie wa chama cha UDM amehifadhi kiti chake katika wadi ya Ileret kwa kupata kura 1,529.