Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Na Grace Gumato
Mwanaume mmoja kutoka Loiyangalani amehukumiwa miaka 5 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12 mwaka uliopita.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Marsabit Simon Arome amesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mbele yake kuwa mtuhumiwa alitekeleza unyama huo.
Puna Erot alikamatwa na kushtakiwa kwa kumdhalilisha kingono msichana huyo katika kijiji cha Yoro, Loiyangalani tarehe 18 Novemba 2021.
Erot alikana shtaka mbele ya hakimu Simon Arome wa mahakama ya Marsabit akitaka kuachiliwa.
Wakati huo uo Abudo Elema Magado amefikishwa katika mahakamani iyo hiyo kwa kosa sawa na hilo la ubakaji.
Anadaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 katika eneo la Elbeso kaunti ndogo ya North Horr.
Aidha, mshukiwa huyo ameshtakiwa kutenda kosa hilo mnamo tarehe 28 mwezi uliopita-Septemba mwaka huu.
Mshukiwa alikana shtaka hilo huku kesi ikitarajiwa kusikilizwa tarehe 27 mwezi huu mjini North Horr.