Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Na Machuki Dennson
Kello Harsama ambaye amejiuzulu ili kuwania ugavana katika kaunti ya Marsabit amesema anafurahia utendakazi wake katika wizara ya kilimo nchini.
Kello ambaye hadi kujiuzulu kwake alikuwa mkurugenzi wa mamlaka ya kilimo na vyakuloa nchini AFA amesema anafurahia anapoondoka kwa sasa bei ya sukari na ile ya unga wa ngano ipo juu kabisa.
Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Kenya bei ya sukari na hata unga ngano zipo juu Zaidi huku wakenya wakilia kulemewa na uchumi.
Kulingana na Kello bei hizo za juu ni manufaa kwa wakulima wa miwa na hata ngano.
Kello alijiuzulu siku ya Jumanne ili kurejea Marsabit kukabiliana na gavana wa sasa Mohamud Ali ambaye anatafuta kusalia mamlakani.
Kello maajuzi naye aliidhinishwa na wazee wa Baliti kule Sololo kuwania ugavana wa Marsabit.
Anasema ana tajriba ya kutosha katika kazi za umma.