Local Bulletins

Basi labingiria mtoni na watu 43 kule Kisii, mtu mmoja afariki

Basi la Modern Coast lililoanguka Kisii

 

Na Machuki Dennson

Mtu ameaga dunia katika ajali ya barabarani asubuhi ya leo katika kaunti ya Kisii.

Basi hilo la Modern Coast lilikuwa likirejea nyuma ili kuegeshwa kabla ya kuteleza na kuanguka mtoni.

Aliyeaga dunia hakuwa abiria katika basi hilo ila mtu aliyegongwa na basi wakati liliteleza. Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Kisii Amos Ambasa amethibitisha kufariki kwa mtu mmoja licha ya kampuni ya basi hilo kukanusha taarifa hizo mapema leo.

Majeruhi kwa sasa wanaendelea kuuguza majeraha katika hospitali mbali mbali mjini Kisii wakati mwili wa mwendazake ukipelekwa katika makafani ya hospitali kuu ya Kisii.

Basi hilo kwa sasa liko katika kituo cha polisi cha Kisii. Awali kampuni ya Modern coast iliripoti kuwa basi hilo lililokuwa na watu 43 halikusababisha maafa yoyote.

Basi lilikuwa njiani kuenda Homa Bay kutoka Mombasa na lilikuwa likiegeshwa ili libebe abiria Zaidi kuendelea na safari.

Subscribe to eNewsletter