Local Bulletins

Balozi Ukur Yatani hatawania kiti cha ugavana Marsabit

Waziri wa fedha na mipango ya kitaifa Ukur Yatani

Na Machuki Dennson

Waziri wa Fedha nchini Ukur Kanacho Yatani amesema kwamba hatowania kiti chochote mwaka katika ulingo wa siasa.

Waziri Yatani ametoa taarifa yake usiku wa leo wakati wa makataa ya mwisho ya kujiuzulu akisema kwamba hatajiuzulu.

Badala yake Waziri Ukur ameweka wazi kuwa ataendelea kuhudumu katika baraza la mawaziri la rais Uhur Kenyatta hadi mwisho ili kufanikisha mapito kutoka serikali moja hadi nyingine.

Kulingana na Ukur anafahamu umuhimu wa wizara yake kwa nchi na vile vile hali ya uchumi nchini kwa sasa.

Kwenye taarifa yake Ukur amesema kuwa anatambua kuwa watu wa kaunti ya Marsabit wanampenda na wangependa awanie kiti cha ugavana tena ila kwa sasa atawahudumia wanaMarsabit katika ngazi ya kitaifa.

Ameweka wazi kuwa alikuwa na nia ya kuwania tena uongozi wa kaunti hii ili kuikomboa kutokana na uongozi mbaya na matumizi mabaya ya mali ya umma ila kwa sasa amechagua kuendelea kuhudumu katika baraza la rais Kenyatta.

Ukur hata hivyo amewataka wananchi wa Marsabit kuwachagua viongozi waadilifu katika uchaguzi wa mwezi Agosti huku akipigia debe muungano wa Azimio la Umoja.

 

 

 

Subscribe to eNewsletter