Local Bulletins

Waziri Wa Usalama Wa Ndani Daktari Fred Matiangi Akutana Na Viongozi Wa Isiolo,Wajir Na Garrissa.

Waziri Wa Usalama Wa Ndani Daktari Fred Matiangi.
Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Waziri Wa Usalama Wa Ndani Daktari Fred Matiangi Amekutana Na Baadhi Ya Viongozi Wa Kaskazini Mwa Nchini Ili Kutafuta Suluhu La Mizozo Ya Mara Kwa Mara Ambayo Imekuwa Ikishuhudiwa.

Akizungumza Baada Ya Mkutano Huo Ambao Uliwaleta Pamoja Magavana Mohamed Kuti Wa Isiolo, Ali Bunow Korane Wa Garissa Na Mohamed Abdi Mohamud Wa Wajir,Waziri Matiangi Ametaja Kuwa  Wizara Ya Usalama Itakikisha Mizozo Ambayo Imekuewa Ikishuhudiwa Katika Mipaka Ya Kaunti Hizo Imesitishwa.

VileVile Matiangi Amesema Kuwa Serekali Pia Hatamsaza Kiongozi Yeyote Atakaye Patikana Kuchochea Jamii.

Aidha Viongozi Hao Walikubaliana Kufanya Kazi Kwa Pamoja Na Serekali Kuu Ili Kutafuta Suluhu La Kudumu.

Itakubukwa Kuwa Watu Kadhaa Wamepoteza Maisha Yao Katika Siku Za Hivi Maajuzi Kutoka Na Mizozo Inayoshuhudiwa Mipakani Mwa Kaunti Hizo, Chanzo Kikuu Kikitajwa Kuwa Mzozo Wa Raslimali Mbalimbali.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter