Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Silvio Nangori
Wanyamapori wameripotiwa kuathirika Zaidi kufuatia Kiangazi kinachoendelea kushuhudiwa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi na kulemaza shughuli ya Shirika la kulinda wanyamapori.
Ukosefu wa mvua katika maeneo mengi kama vile kaunti ya Marsabit, Isiolo Wajir na Garissa, kumeripotiwa kuaga dunia kwa wanyama pori.
Hali hiyo inadaiwa kuwa huenda ikawa mbaya zaidi iwapo taifa litashuhudia mvua kiwango cha chini kama ilivyoripoti idara ya utabiri ya hali ya anga. Ameiambia Radio Jangwani Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Wanyamapori KWS, eneo la Mashariki mwa Kenya Robert Obrein.
Baadhi ya wanyamapori kama vile Twiga, paa na Nyati katika maeneo ya Garissa, Wajir, Tana River na sehemu za Mbuga za ufugaji wa wanyamapori za Meru wameripotiwa kuaga maajuzi.
Majira ya ukavu wa kiangazi yamechangia pakubwa katika migogoro kati ya wafugaji na wanyamapori kwa ajili ya uhaba wa nyasi na maji.
Obrein amesema kwamba KWS ilipata changamoto kutoka kwa jamii za wafugaji walio katika maeneo yale ambapo ngamia na Ngombe wamekuwa wakiingia katika mbuga kulisha mifugo yao haswa maeneo ya Garissa na Wajir.