Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya
Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Marsabit wanafaa kuwajibikia swala la usalama kikamilifu na kuhubiri Amani katika mikutano yao.
Hayo ni kwa mujibu wa muaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo mbunge la Saku mwaka wa 2022 Abdub Barrille.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bariille amesema kuwa wanasiasa katika kaunti ya Marsabit wana ufahamu wa kutosha kuhusiana na yote ambayo yamekuwa yakijiri katika kaunti hii bila kuwajibika ila tu kunyoosheana lawama.
Barrille na ambaye kwa wakati mmoja alimuunga mkono Gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali ameonekana kulenga vinginevyo huku akitaja kuwa Gavana Ali amefeli katika kuwahakikishia wananchi wa jimbo hili usalama wa kutosha na vilevile mazingira bora ya kufanyia Kazi.
Aidha Barrille amewataka wa wananchi kutotumiwa vibaya na wanasiasa na badala yake kuwa na misimamo dhabiti haswa kuhusiana na swala la usalama jimboni.