Local Bulletins

Wakenya Wametakiwa Kutoingiza Siasa Swala La Kukabiliana Na Ufisadi Nchini.

Picha; Hisani

By Waihenya Isaac

Wakenya wametakiwa kutoingiza siasa swala la kukabiliana na ufisadi nchini na badala yake kupiga jeki zoezi hilo kwa kupiga ripoti wanaposhuhudia visa vyovyote vya ufisadi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume  ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC Eliud Wabukala ni kuwa vita dhidi ya ufisadi vinahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi na pia idara mbali mbali za  serekali ili kuzaa matunda.

Wabukala aliyasema hayo alipokuwa akihutubia kongamano la MaMCAs nchini linaloendelea kwa sasa mjini Mombasa.

Aidha Wabukala amewataka MaMCAs kudumisha maadili mema na kuwa kielelezo kwa jamii.

Vilevile Wabukala amelaani kisa cha hivi maajuzi ambapo wawakilishi wadi wa kaunti ya Baringo walirushiana Makonde Bungeni wakti wa kujadiliwa kwa mswada wa marekebisho ya Katiba BBI.

Subscribe to eNewsletter