Local Bulletins

Wabunge Sylvanus Osoro Na Simba Arati Waorodheshwa Katika Orodha Ya Aibu Iliyotolewa Na Tume Ya Uiano Na Utengamano Nchini NCIC.

Picha; Hisani

By Waihenya Isaac,

Tume ya uiano na utengamano Nchini NCIC imetoa onyo kwa wanasiasa wanaotumia mazishi kama jukwa la kueneza chuki baina ya wananchi.
Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa tume hiyo Samuel Kobia amesema kuwa NCIC itahakikisha kuwa wananchi wanadhibitiwa ili kuzuia mgawanyiko Nchini.
Kadhalika Tume hiyo imetoa orodha ya wanasiasa waliokatika orodha ya Aibu na wale waliofanya juhudi za kuhubiri Amani nchini, huku ikiwataka wananchi kukataa kutumiwa na wanasiasa kueneza chuki baina ya jamii hususan Katika kipindi hichi taifa linaelekea Katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika orodha hiyo ya viongozi walioleta fedheha katika jamii ni akiwemo Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko anakabiliwa na mashtaka kwa sasa.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter