Local Bulletins

TSC Yakana Madai Ya Njama Kuwahamisha Walimu Haswa Katika Ukanda Wa Kaskazini Mwa Nchi.

Katibu Mkuu Mtendaji Wa Tume Ya Huduma Za Walimu Nchini TSC Bi Nancy Macharia

By Jillo Dida Jillo,

Tume ya kuwajiri waalimu Nchini TSC imekana madai kuwa imekuwa ikipanga hamisho za walimu kote nchini haswa katika ukanda wa kazkazini mwa nchi.

Katika taarifa yake TSC imesema kuwa ripoti ya Arafa iliyotelewa ilikuwa ni ya kutoa mwelekeo mzuri kwa tume japo sio ya kuhamisha walimu.

Awali TSC kupitia kwa afisa mkuu mtendaji Nancy Macharia alitangaza kuwa kabla ya kufunguliwa kwa shule mnamo Januari 2021 kwamba haingeweza kuhamisha walimu kwa wingi mwaka huu kutokana na changamoto za corona ambazo zimeadhiri kalenda ya masomo.

Hata hivyo pendekezo la awali ya TSC imepingwa vikali na kamati ya bunge la kitaifa

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter