Local Bulletins

TSC Kuwapandisha Vyeo Walimu Takriban Elfu Moja.

Katibu Mkuu Mtendaji Wa Tume Ya Huduma Za Walimu Nchini TSC Bi Nancy Macharia

By Radio Jangwani,

Tume ya Huduma za Walimu, TSC imetangaza rasmi nafasi elfu moja za kuwapandisha vyeo walimu kuanzia mwezi ujao wa Februari

TSC inalenga kuwapandisha vyeo walimu 492 wa shule za upili walio chini ya kitengo cha kwanza cha kazi T-scale 8.

Aidha walimu wengine ni mia tatu sitini na watatu wa kitengo cha nne cha kazi T-scale 9.

Tume hiyo vile vile,  imetangaza kuwapandisha vyeo walimu sabini na wawili kuwa manaibu walimu wakuu na wengine kumi na watano kuwa walimu wakuu huku ishirini na wanane wakiwa wahadhiri wakuu.

Afisa Mkuu Mtendaji waTSC, Nancy Macharia amewashauri walimu wanaolenga kupandishwa vyeo kutuma maombi kuambatana mwongozo wa maendeleo ya taalumu ya ualimu.

 

Subscribe to eNewsletter