Local Bulletins

Ni lazima katiba itabadilishwa – Asema Babu Owino.

Mbunge wa Embakasi ya mashariki Babu Owino.
Picha;Hisani

Na Adano Sharawe,

Mbunge wa Embakasi ya mashariki Babu Owino ametangaza kuwa ni lazima  katiba itabadilishwa.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, mbunge huyo anayekumbwa na sarakasi si haba siasani amesema hawatorudi nyuma kwenye nia yao ya kubadilisha katiba kupitia mswada wa BBI.

Babu ametangaza matamshi haya siku moja baada ya mahakama kuu ya Kenya kutupilia mbali mchakato mzima wa BBI.

Siku ya Alhamisi, mahakama ilikosoa hatua ya Rais Kenyatta kuongoza mchakato wa BBI huku majaji wakidai kuwa shughuli hiyo ilifaa kumilikiwa na wananchi na wala sio rais mwenyewe.

Majaji hao pia walikosoa hoja ya kuongeza maeneo bunge sabini huku wakiashiria kuwa kisheria hiyo ni kazi ya tume ya IEBC wala sio jopo lililoteuliwa na Rais.

Babu Owino ambaye ni mwandani mkubwa wa kinara wa ODM, Raila Odinga amekuwa kwenye mstari wa mbele katika kupigia debe mchakato wa BBI.

 

Subscribe to eNewsletter