Local Bulletins

Mwanaume Mmoja Ahukumiwa Kifungo Cha Miaka 44 Kwa Kosa La Kumdhulumu Mpwa Wake Kigono.

 

Picha;Hisani

By Samuel Kosgei,

Mahakama ya Machakos imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 44 kwa kosa la kumdhulumu mpwa wake 10 kigono mwaka wa 2017.

Mahakama awali iliambiwa kuwa Mvulana huyo aliaga dunia baadaye alipofikishwa katika makao ya kunusuru watoto mjini Machakos.

Nicholas Kioko Mutisya alipatwa na kosa la kumdhulumu mvulana huyo December mwaka 2017 na wiki ya kwanza ya January 2018.

Kitendo hicho kilifanyika katika kijiji cha Muisuni village, kaunti ndogo ya Mwala kauti hiyo ya Machakos.

Uamuzi huo ulifanywa jana na hakimu mkuu wa mahakama hiyo Ann Wanyoike.

Ann alitoa uamuzi huo akionya wanaume wanaotenda vitendo kama hivyo vya kinyama. Yeyote anayekutwa na kosa la kudhulumu kigono au kufanya mapenzi na watoto chini ya miaka 11 hufungwa maisha gerezani.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter