Local Bulletins

Mwanafunzi Wa Kidato Cha Tatu Katika Shule Ya Wavulana Ya King David Kamama Katika Kaunti Ya Embu Apatikana Na Risasi Shuleni.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Mwanafunzi wa kidato cha tatu Katika shule ya wavulana ya King David Kamama Katika kaunti ya Embu aliyepatikana akiwa na risasi  pamoja na mwenzake aliyepatikana akijaribu kutetekeza Bweni wanazuiliwa Katika kituo cha polisi cha Manyatta  kaunti ya Embu.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Katika kaunti hiyo Daniel Rukunga kuwa  kuwa njama ya kuteketeza Bweni la shule ilitibuliwa na mlinzi wa shule baada ya kuwashuku wanafunzi kadhaa na walipoitwa ili kukaguliwa ndipo mmoja akapatikana na risasi ya milimita 7.6 inayoweza kutumika Katika bunduki kama AK 47.

Wakti uo huo wasichana 24 ambao walikamatwa Katika shule ya upili ya wasichana ya Ndagaiya kauti hiyo ya Embu wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani mjini Runyenjes hii leo.

Wasichana hao pamoja na mfanyikazi mmoja wa shule hiyo wanakabiliwa na mashtaka ya uteketezaji wa shule.

 

Subscribe to eNewsletter