Local Bulletins

Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 17 auwawa katika hali tatanishi huko Wajir.

Picha:Hisani

By Waihenya Isaac,

Wingu la simanzi limetanda katika mji wa Wajir baada ya mvulana mwenye umri wa miaka kumi na saba kuuwawa katika hali tatanishi.

Mwili huyo wa mvulana kwa jina Abei Bishar ulipatikana katika eneo la Stage Driftu usiku huku ukiwa na jereha la kisu shingoni na kuvuja damu.

Aidha mwili wake ulizikwa katika makaburi ya Almaho mjini Wajir kulingana na dini yake.

Akidhibitisha kisa hicho OCPD wa Wajir mashariki Kennedy Samani amesema kuwa tayari uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Samani hata hivyo ametoa wito kwa wakaazi wa eno hilo kuwa wangalifu na hata kutoa taarifa kwa maafisa wa usalama endapo watakutana na visa vya uhalifu.

 

Subscribe to eNewsletter