Local Bulletins

Mswada kuhusu dawa za kulevya kurejeshwa Bungeni – wakati huu ukiwa na vipengee vinavyopendekeza adhabu kali zaidi.

Picha;Hisani

Na Waihenya Isaac,

Rais Uhuru Kenyatta ana mpango wa kurejesha mswada wa mwaka jana bungeni kuhusu dawa za kulevya, wakati huu ukiwa na vipengee vinavyopendekeza adhabu kali zaidi.

Tayari baadhi ya wabunge wamepongeza hatua hii lakini kwa wakati huo akaomba mswada huo upigwe msasa ili uzingatie zaidi kumsaidia mraibu kurekebika kuliko kumuadhibu na kifungo.

Sheria hii inapania kuharamisha umaskini kwa kuadhibu waraibu na ambao kwa idadi na wana kipato cha chini ilhali walanguzi wakuu ambao ni mabwenyenye wakiwa na mwanya wa kutoadhibiwa.

Kwa mujibu wa mswada huo wanaopatikana na mihadarati chini ya gramu moja wanakabiliwa na faini ya shillingi millioni tano au kifungo cha miaka mitano au zaidi gerezani.

Subscribe to eNewsletter