Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Samuel Kosgei
Wakaazi wa Lokesheni ya Hurii Hills eneobunge la North Horr wanakadiria hasara kubwa baada ya mifugo Zaidi ya 500 kufa kutokana na upepo mkali uliondamana na mvua kiasi siku ya Jumamosi.
Kulingana na naibu chifu wa lokesheni ya Hurri Hills Roba Abudo ni kuwa wafugaji wengi wanakadiria hasara kutokana na dhoruba hiyo kali.
Ametoa wito kwa asasi za msaada jimboni kuwapa msaada familia zilizoathirika.
Mamo Konchora mmoja wa waathiriwa anasema kuwa kutokana na hali hiyo familia yake imerudi nyuma kutokana na hasara aliyopata yeye na majirani zake.
Wakti uo huo chifu Roba ameomba serikali ya kaunti kujitokeza na kusaidia wakaazi wa Hurri Hills kwa kuwapa maji ya kutumia sawia na mifugo yao kwani kwa sasa watu na mifugo yao wanaumia kutokana na ukosefu wa maji.
Anasema kuwa kwa sasa wakaazi hao wanauziwa mtungi moja wa lita ishirini kwa shilingi 70 suala analosema linaumiza wakaazi kutokana na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu.