Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Adano Sharawe,
Kundi moja la mashirika ya kijamii limetoa wito kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za matumizi ya pesa za serikali akague mara moja pesa za umma zilizotumiwa kufadhili shughuli za mchakato wa BBI na kuwachukulia hatua walioidhinisha matumizi ya pesa hizo.
Kundi hilo linadai kwamba kwa vile mahakama kuu ilipitisha uamuzi kwamba shughuli hiyo ilifanywa kinyume cha katiba, maafisa walioidhinisha matumizi ya pesa hizo za umma lazima waziwajibikie.
Kundi hilo pia linawashutumu wanasiasa kwa kutoridhishwa na uamuzi huo wa mahakama kuu.
Juma lililopita jopo la majaji watano likiongozwa na Prof. Joel Ngugi lilitaja mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa kuwa kinyume cha katiba.
Hatua hiyo ya mahakama kuu ya kutaja mchakato huo kinyume cha sheria,imeibua hisia kali za kisiasa hapa nchini huku wanaounga mchakato huo wakikashifu hatua hiyo.