Local Bulletins

Mali Ya Dhamani Isiyojulikana Imeteketea Baada Ya Moto Kuchoma Ofisi Na Bunge La Kaunti Ya Garissa.

Moto Wachoma Ofisi Na Bunge La Kaunti Ya Garissa.
Picha; Hisani

By Samuel Kosgei,

Mali ya dhamani isiyojulikana imeteketea baada ya moto kuchoma ofisi na bunge la kaunti ya Garissa.

Inaripotiwa kuwa Moto mkubwa ulianza kuonekana katika jengo hilo majira ya saa mbili unusu asubuhi ikitajwa kuharibu bunge lenyewe na ofisi za idara mbalimbali bungeni.

Kulingana na kiongozi wa wachache katika bunge hilo Mohamed Ali, ni kuwa bado chanzo cha moto haujafahamika ila anasema kuwa karibia asilimia 40/50 ya jengo hilo limechomeka.

Viongozi wa bunge hilo wamesema kuwa licha kutofahamu chanzo cha moto huo mafisa wa zima moto na jeshi lilifika kuzima moto huo ambao wameutaja kama kitu ambacho kitawarejesha nyuma.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter