Local Bulletins

Katibu Mkuu wa KNUT Wilson Sossion ndiye chanzo cha masaibu ya chama hicho asema Lufre Gambare

Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion. Picha hisani ya KNUT

Na Isaac Waihenya

Uteuzi wa Wilson Sossion kama mbunge maalumu njdio chanzo cha migogoro kati ya tume ya kuwaajii walimu nchini TSC na muungano wa kutetea haki za walimu nchini KNUT.

Haya ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wa Muungano Wa Waalimu Nchini KNUT Tawi La Marsabit Lufre Gambare.

Gambare akizungumza na Radio Jangwani afisini kwake amesema kwamba Katibu mkuu wa KNUT kote nchini Wilson Sossion alifaa kujiuzulu kutoka wadhifa huo mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mbunge.

Hii ni kutokana na kwamba tangu alipoteuliwa Sosion kuwa mbunge wanachama wengi wa KNUT wamejiondoa chamani kwa kile kinachotazamwa kama kinachochewa na tume ya kuwaajiri walimu TSC.

Gambare anasema ana matumaini kwamba wanachama wao ambao wamehamia muungano wa  walimu pia wa KUPPET watarejea chamani kuanzia mwezi Juni mwaka huu wakati viongozi wa sasa wa KNUT watabanduliwa afisini wote.

Gambare Ameisuta TSC Kwa Kile Alichokitaja Kuwa Njama Ya Kuwahujumu Walimu Kwa Kumaliza Nguvu Muungano Wa KNUT Ambao Umekuwa Katika Mstari Wa Mbele Kutetea Maslahi Ya Walimu Nchini.

Amesema Kuwa TSC Imekuwa Ikiichezea KNUT Shere Kwa Kubadili  Baadhi Ya Makubaliano Katika Yao ila ameshikilia kuwa TSC haitafaulu katika kuusambaratisha muungano wa KNUT.

Kadhalika Gambare Amesifia Swala La Shule Kufunguliwa Akisema Kuwa Wengi Wao Walipotoka Kimaadili wakti wa Likizo Ndefu Ya Korona.

Afisa huyo wa KNUT hapa Marsabit Ameikashifu Wizara Ya Elimu Kwa Kuwazuia Waandishi Wa Habari Kupata Habari Muhimu Katika Shule Za Umaa.

Ametaja Kuwa Wizara Hiyo Haikuwa Imejiandaa Kikamilifu Kwa Ufunguzi Wa Shule Na Hivyo Kuwanyima Wandishi Wa Habari Nafasi Ya Kubaini Hali Halisi.

Subscribe to eNewsletter