Local Bulletins

JSC Yaorodhesha Watu 10 Watakaohojiwa Ili Kujaza Pengo La Jaji Mkuu Aliyestaafu David Maraga

 

 

Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga akiaga idara ya mahakama nje ya majengo ya mahakama ya Juu. Picha;Hisani

By Waihenya Isaac

JSC imewaorodhesha watu 10 watakaohojiwa ili kujaza pengo la jaji mkuu aliyestaafu David Maraga.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari,tume hiyo pia imewaorodhesha watu wengine 9 watakaohojiwa kwa  nafasi ya jaji wa mahakama ya upeo.

Walioorodheshwa kwa nafasi hiyoni pamoja na  Jaji Said Chitembwe, Prof Patricia Mbote,Jaji Martha Koome, Jaji Marete Njagi,Wakili Philip Murgor,Jaji Nduma Nderi, Wakili Fred Ngatia,Jaji William Ouko,Daktari Wekesa Moni na Alice Yano.

Majaji wote wa mahakama ya upeo akiwemo kaimu jaji mkuu Philomena Mwili hawakutuma maombi ya kazi hiyo ili kumrithi jaji mkuu mstafuu David Maraga

Walioorodheshwa kuhojiwa kwa nafasi ya jaji wa mahakama ya upeo ni Jaji Said Chitembwe, Jaji Martha Koome, Jaji M’inoti Kathurima,Jaji Nduma Nderi, Lumumba Nyaberi,Jaji William Ouko,Jaji Joseph Sergon  na  Alice Yano.

Wananchi wametakiwa kutuma maoni yao kuwahusu waliotuma maombi ya kazi hizo kufikia machi tarehe 31.

Tume hiyo inalenga kuziziba nafasi  zilizoachwa na  David  Maraga na Jaji Jackton Ojwang’ aliyekuwa jaji wa mahakama ya upeo .

 

Subscribe to eNewsletter