IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Samuel Kosgey
Taharuki inazidi kushuhudiwa mjini Marsabit na viunga vyake kufuatia kuuawa kwa mtu mmoja siku ya Jumatatu jioni.
Biashara mjini zimeathirika pakubwa kutokana na kulazimika kuungwa mapema na wenyejio kutoroka mjini kwa sababu ya kuwa na hofu.
Kwa sasa mtu mmoja anauguza majeraha baada ya kupigwa risasi kwenye tukio la Jumatatu jioni ambapo mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake katika eneo la African Muslim Agency kwenye barabara kuu ya Marsabit – Moyale hatua chache kutoka mji wa Marsabit.
Marehemu ambaye amezikwa Jumanne katika makaburi ya Marsabit mjini aliauawa baada ya kupigwa risasi na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wakitumia pikipiki.
Mhasiriwa kwa sasa anapokea matibabu katika hospitali kuu ya rufaa ya Marsabit.
Kisa hicho kinajiri siku chache baada ya watu 6 kuuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika mkasa ambapo gari la abiria lilishambuiwa katika eneobunge la saku.