Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Rais Joe Biden ameahidi Kenya kwamba Marekani itatoa msaada wa mara moja wa dozi zaidi ya milioni 17 za chanjo ya Johnson & Johnson kwa Umoja wa Afrika.
Biden alitangaza hayo wakati wa mkutano na rais Uhuru Kenyatta kwenye afisi yake ya Ikulu mjini Washington DC, ambao pia ulijadili ushirikiano katika masuala mbalimbali.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Marekani kutoa msaada wa chanjo za Covid-19 kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, baada ya kutangaza hatua ya kutoa takriban dozi milioni hamsini mwezi Julai mwaka huu.
Tayari chanjo hizo zimetumwa kwa nchi mbalimbali, ikiwemo Kenya ambayo imepokea dozi milioni 2.5 kutoka kwa mpango huo.
Mkutano huo ulikuwa wa kwanza wa Biden akiwa rais, na kiongozi wa Kiafrika.
Rais huyo alisema kwamba Kenya ni mshirika muhimu wa Marekani na amewajibika vilivyo kama kiongozi wa kieneo katika nyanja ya amani na usalama.
Kenyatta alimshukuru Biden kwa kutangaza msaada huo wa chanjo akisema kwamba Afrika imesalia nyuma mno katika utoaji wa chanjo kwa watu wake.