MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Ni afueni sasa kwa wakaazi wa kaunti ya Marsabit waliokuwa wakikosa dawa katika hospitali za umma baada ya dawa kununuliwa na kusambazwa katika hospitali zote za umma wiki mbili zilizopita.
Akizungumza na kituo hiki ofisini mwake waziri wa huduma za afya katika kaunti ya Marsabit Dr. Jama Wolde ameomba wakaazi kufika hospitali za umma ili kupokea huduma za afya bila kuhangaika tena.
Amesema kuwa dawa hizo zimegharimu serikali kima cha shilingi milioni 30.5 na hivyo kusuluhisha tatizo la ukosefu wa dawa ambao umekuwa ukishudiwa kwa muda. Dawa hizo anasema zimesambazwa na shirika kusambaza dawa na vifaa vya matibabu KEMSA.
Aidha ametaja kuridhishwa na idadi ya wakaaji wanaozidi kufika hospitalini kupokea chanjo dhidi ya virusi vya corona. Kulingana naye Zaidi ya watu 1600 tayari wamepokea chanjo hiyo kufikia sasa.