Mapacha wauliwa Dukana, Marsabit kutokana na Imani kuwa wataletea familia ‘Nuksi’.
January 22, 2025
Na Samuel Kosgei
Kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Robinson Mboloi amepiga marufuku uendeshaji wa bodaboda katikati ya mji wa Marsabit na viunga vyake kutokana na ongezeko la visa vya mauaji kutumia pikipiki.
Kisa cha hivi punde cha mauaji ni kisa ambapo watu wawili wameuliwa na watu waliokuwa kwenye pikipiki mchana wa hiyo jana Alhamisi.
Akizungumza na wanahabari ofisini mwake, Mboloi amesema kuwa kamati ya usalama mjini marsabit imeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia ongezeko la mauaji ya kila mara.
Mboloi anasema kuwa kuanzia mwezi Novemba watu Zaidi ya 10 wameuawa kwa mtutu wa bunduki na watu wanaotoroka kutumia pikipiki.
Kauli yake Mboloi inajiri baada ya watu wawili kuuliwa hii kwa kupigwa risasi katika eneo la Dakabaricha na Nagayo viunga vya mji wa Marsabit.
Kamanda ametoa wito kwa wanamarsabit kutoa habari dhidi ya uhalifu kwa maafisa wa polisi ili kuzuia mauaji kabla ya kufanyika.
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 56 amethibitishwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana maeneo ya Majengo muda ya saa kumi na mbili jioni siku ya Jumatano.
Akidhibitisha kisa hicho kamanda wa polisi Robinson Mboloi amesema kuwa watu waliokuwa wamejihami na bunduki walimpiga mzee huyo kwenye kichwa na kisha kutoweka.