Local Bulletins

ANN KANANU HALALI AFISINI KAMA NAIBU GAVANA KAUNTI YA NAIROBI

Naibu gavana na kaimu gavana wa kaunti ya Nairobi. Picha hisani

NA MACHUKI DENNSON
MAHAKAMA imeidhinisha uteuzi na kuapishwa kwa Ann Kananu kama naibu gavana wa kaunti ya Nairobi. Jopo la majaji watatu jioni hii wameamuru kwamba uamuzi wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kubatilisha uteuzi wa Kananu ulikuwa na nia ya kuhujumu utendakazi wa kaunti hiyo ya Nairobi. Majaji hao katika uamuzi wamesema kwamba mara baada ya Sonko kumteua Kananu kama naibu wake, hakuwa tena na uamuzi wa kubatilisha uamuzi huo bila ya kuhusisha bunge la kaunti hiyo. Sonko ambaye alitimuliwa kama gavana wa Nairobi katika kesi hiyo alikuwa akipinga kuwa Kananu hakufaa kuanza kutekeleza majukumu ya naibu gavana kwa madai kuwa tayari alikuwa amebatilisha uteuzi wake. Ushahidi uliotolewa mahakamani na mawakili wa Kananu unaonyesha kuwa Sonko alijaribu kubatilisha uteuzi wa Kananu alipotimuliwa na bunge la kaunti. Majaji Said Chitembwe, Wilfrida Okwany na Weldon Korir kwa pamoja wameamuru kuwa spika wa bunge la kaunti ya Nairobi alikubaliwa kisheria kuanzisha mchakat wa kumpiga msasa na hata kumwapisha naibu gavana ambaye jina lake lilikuwa limependekezwa na gavana alipokuwa afisini.

Subscribe to eNewsletter