Local Bulletins

Wanaopania Kuwania Kiti Cha Gavana Wa Nairobi Wanahadi Leo Jioni Kuwasilisha Nyaraka Zao Kwa IEBC.

Picha; Hisani.

By Waihenya Isaac

Wanaopania Kuwania Wadhifa Wa Gavana Wa Kaunti Ya Nairobi Wanahadi Leo Jioni Kuwasilisha Nyaraka Zao Kwa Tume Huru Ya Uchaguzi Na Mipaka IEBC.

Kwa Mujibu Wa IEBC, Vyama Vya Kisiasa Vinavyokusudia Kushiriki Katika Uchaguzi Huo Mdogo, Vinafaa Kuwasilisha Majina Ya Wagombea Wao Ifikikiapo Leo Jioni.

Aidha IEBC Imesema Kuwa Wagombea Wanaokusudia Kushiriki Katika Uchaguzi   Huo Mdogo Kama Wagombeaji Huru Pia Wanafaa Kuwasilisha Majina Na Alama Zao Ambazo Wanakusudia Kutumia Wakati Wa Uchaguzi.

Wiki Jana IEBC Ilitenga Februari 18, 2021 Kuwa Siku Ya Uchaguzi Mdogo Wa Kaunti Ya Nairobi Kumtafuta Gavana Atakayechukua Nafasi Ilioachwa Wazi Na Mike Sonko, Baada Ya Bunge La Seneti Kuidhinisha Mwaada Wa  Kumbandua  Ofisini Uliokuwa Umepitishwa Na Bunge La Kaunti Ya Nairobi.

 

Baadhi Ya Wanaomezea Mate Kiti Hicho Ni Ikiwemo Aliyekuwa Gavana Wa Kiambu William Kabogo, Miguna Miguna,Askofu Magreat Wanjiru, Peter Kenneth  Na Wengine Wengi.

Hata Hivyo Wafanyakazi Wa Umma Wanaopania Kuwania Nafasi Wanafaa Kujiuzulu Kutoka Ofisi Hizo Za Umma Katika Kipindi Cha Siku Saba Tangu Nafasi Hiyo Kutangazwa Kuwa Wazi.

Uteuzi Wa Vyama Unafaa Kufanyika, January 18 Na January 19, 2021.

IEBC Aidha Imesema Kuwa Kipindi Cha Kampeni Itaanza January 18, Na Kumalizika February 15, 2021.

Subscribe to eNewsletter