Local Bulletins

Upepo Ulioandamana Na Mvua Wang’oa Paa Ya Darasa Moja Na Ofisi Ya Walimu, Katika Shule Ya Upili Ya Helu Eneobunge La Moyale.

Picha: Hisani

Na Samwel Kosgei,

Shule Ya Upili Ya Helu Iliyoko Eneobunge La Moyale Kaunti Hii Ya Marsabit Inakadiria Hasara Ya Maelfu Ya Pesa Baada Ya Upepo Iliyoandamana Na Mvua Kung’oa Paa Ya Darasa Moja Na Ofisi Ya Walimu.

Akizungumza Na Shajara Ya Jangwani Kwa Njia Ya Simu Mwalimu Wa Shule Hiyo Rob Galgallo Amesema Kuwa Ofisi Ya Walimu Iliyotumika Kama Maabara Ya Sayansi Ilibomolewa Na Hivyo Kuathiri Vifaa Vya Masomo.

Aidha Mwalimu Galgallo Amesema Hapakuwa Na Majeruhi Yoyote Kwa Mkasa Huo Uliotokea Jumatano Mchana Licha Ya Wanafunzi Wa Kidato Cha Nne Kuwa Shuleni.

Ametoa Wito Kwa Mbunge Wa Moyale Qalich Gufu Kusaidia Shule Hiyo Kurejelea Hali Yake Ya Kawada Kupitia Hazina Ya Maendeleo Ya Eneo Bunge (CDF) Kabla Ya Wanafunzi Wengine Kurejea Shuleni Mwezi January.

 

Subscribe to eNewsletter