Local Bulletins

NCIC Yaapa Kuwachukua Hatua Kali Wanasiasa “Ambao Watavunja Sheria” Wakati Wa Chaguzi Ndogo Zijazo.

Mwenyekiti Wa Tume Ya NCIC Samwel Kobia.
Picha; Hisani

By Waihenya Isaac

Tume Ya Uwiano Na Utangamano  Nchini NCIC Imeapa Kuwachukua Hatua Kali  Wanasiasa “Ambao Watavunja Sheria” Wakati Wa Chaguzi Ndogo Zijazo.

Kupitia Mwenyekiti Wake  Samuel Kobia NCIC  Imetaja Kuwa Imepata Funzo Katika Uchaguzi Mdogo Wa Msambweni, Ambao Uligubikwa Na Cheche Za Chuki Katika  Kipindi Cha Kampeni.

Kobia Ameahidi Kuwa NCI Itawaadhibu Wanasiasa Ambao Watatishia Amani U Na Husiano Mzuri  Katika Jamii.

Mapema Wiki Hii NCIC Ilimwita Katibu Mkuu Wa Chama Cha ODM Edwin Sifuna Na Mbunge Wa Malindi Aisha Jumwa Sifuna Kurekodi Taarifa Juu Ya Matamshi Machafu Waliyotoa Wakti Wa Kampeni Za Uchaguzi Mdogo Wa Msambweni.

Wawili Hao  Waliomba Msamaha Kwa Matamshi Hayo Na Kuahidi Kujizuia Katika Siku Zijazo.

Matamshi Ya Kobia Yanajiri Wakti Tume Huru Ya Uchaguzi Na Mipaka Nchini IEBC Inajiandaa Kwa Uchaguzi Mdogo Katika Kaunti Ya Nairobi Na Eneo Bunge La Matungu.

Wakaazi Wa Nairobi Wataelekea Kupiga Kura Mnamo Februari 18, 2021, Kumchagua Gavana Mwingine Kufuatia Kubanduliwa Kwake Gavana  Mike Sonko Huku Tarehe 4 Mwezi Machi Mwaka Ujao Wakaazi Wa Eneo Bunge La  Matungu Wakitarajiwa Kumchangua Mbunge Mpya Baada Ya Aliyekuwa Mbunge Justus Murunga Kuaga Dunia.

Kadhalika IEBC Inasubiri Viti Vya Machakos Na Kabuchai Kutangazwa Wazi Kufuatia Kifo Cha Seneta Boniface Kabaka Na Mbunge James Mukwe Lusweti Mtawaliwa.

Subscribe to eNewsletter