Local Bulletins

Magavana Jackson Mandago Na Stephen Sang Wamtaka Rais Uhuru Kenyatta Kumfuta Kazi George Kinoti.

 

By Waihenya Isaac,

Viongozi Kutoka Eneo La Bonde La  Ufa Wanamtaka  Rais Uhuru Kenyatta Kumfuta Kazi Mkurugenzi Mkuu Wa Upelelezi  Wa Jinai DCI George Kinoti Kwa Kujaribu Kufufua Kesi Za Ghasia Za Baada Ya Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka Wa 2007/2008.

Wakiongozwa Na Gavana Wa Uasin Gishu Jackson Mandago Na Stephen Sang Wa Nandi, Viongozi Hao Wanamtaka Kinoti Kuomba Umma Msamaha Kwa Kutonesha Vidonda Vyao Vilivyopona.

Photo Coutersy,

Aidha Wawili Hao Wamedai Kuwa Wangetaka Serekali Kubaini  Madai Kuwa DCI Iliwashinikiza Waadhiriwa Wa Ghasia Hizo Kuandikisha Taarifa.

Kulingana Nao Kinoti Alitishia Amani Ya Taifa Na Hafai Kuendelea  Kushikilia Wadhifa Huo Wakati Wa Uchaguzi Wa Mwaka Mkuu Wa Mwaka 2022.

Hata Hivyo, DCI Ilibainisha Kuwa Lengo Kuu Halikuwa Kufufua Kesi Za Ghasia Za  Baada Ya Uchaguzi Wa Mwaka 2007/2008 Bali Inapania Kuchunguza Madai Ya Waadhiriwa Kutishiwa Maisha.

Photo Coutersy,

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter