Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Aliyekuwa askofu wa jimbo la Meru kati ya mwaka 1976 hadi mwaka 2004, askofu Silas Silvius Njiru ameaga dunia.
Marehemu askofu Njiru aliaga dunia usiku wa kuamkia jana Jumanne saa sita usiku nchini Italia. Kifo chake kimetokana na maambukizi ya virusi vya corona mjini Turin Italia alikokuwa akiishi katika nyumba ya maaskofu wastaafu wa shirika la Consolata, Mbarikiwa Alamano.
Taarifa ya katibu mkuu wa shirika la waconsolata ulimwenguni padre Pedro Jose Da Silva Louvo imesema kwamba marehemu askofu Njiru aliugua na kupelekwa hospitalini tarehe 25 mwezi huu wa Aprili na kutokana na corona akathibitishwa kuaga dunia saa sita unusu usiku wa kuamkia Jumanne katika hospitali ya Rivoli.
Marehemu askofu Njiru alizaliwa mnamo mwaka 1928 tarehe 10 mwezi wa kumi jimbo la Meru. Mwaka 1955 alitawazwa kuwa padre na mwaka 1975 akateuliwa kuwa askofu msaidizi wa jimbo la Meru na msimamizi wa jimbo la Maturba nchini Algeria.
Mwaka mmoja baadaye alitawazwa rasmi kuwa askofu wa jimbo la Meru hadi mezi Machi mwaka 2004 alipostaafu kama askofu.