Mfumo wa kutatua kesi nje ya mahakama (AJS) wazinduliwa rasmi,Marsabit.
November 23, 2024
By Samwel Kosgey
Washukiwa 11 kati ya 22 wa uvamizi wa kituo cha polisi cha Kargi ijumaa wiki jana wameachiliwa huru.
Afisa wa polisi anayeongoza uchunguzi huo Albert Juma ameiambia mahakama kuwa amewaondolea mashtaka Washukiwa 11 kwa kukosekana ushahidi dhidi yao.
Hata polisi wamewafungulia mashtaka washukiwa watatu kwa kumiliki silaha kinyume na sheria.
Watatu hao Ilbayo Narogo, Rira Baro na Sunyai Baro wameshtakiwa kwa kumiliki bunduki na risasi bila kibali.
Washukiwa hao wameachiliwa kwa bondi ya shilingi elfu 300 kila mmoja au mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Wakili wa serikali Dedan Kihara ameiambia mahakama kuwa watatu hao kumiliki bunduki kinyume cha sheria ni makosa na walihatarisha maisha ya wananchi na polisi haswa usiku huo wa uvamizi. Katika kesi hiyo washukiwa wengine wanane wameshtakiwa kwa kumtorosha mfungwa. Mahakama imewaachilia wanane hao kwa dhamana ya shilingi 1000 moja kila mmoja.
Wakili wa washtakiwa Kevin Nyenyire amesema ameridhishwa na kuachiliwa kwa 11 bila mashtaka na bondi ya 1000 kwa wengine wanane sio mbaya.
Kuhusiana na watatu walioshtakiwa kwa makosa ya bunduki Nyenyire amesema kuwa shtaka lao ni zito na kuachilia kwa bondi ya laki tatu ni wastani.
Mbunge wa Laisamis Musa Arbele kwa upande wake amesema kuwa wao kama viongozi wataendelea kuhamasisha jamii na vijana haswaa dhidi ya hulka ya kutofuata sheria na kuvamia polisi. Kesi hiyo itatajwa tarehe 6 aprili.