Local Bulletins

AFISA WA POLISI AJIUA, DUKANA

Gari la Maafisa wa Polisi.
Photo: Courtesy.

Na Adano Sharawe.

Afisa mmoja wa polisi katika kambi ya Buluk, kaunti ndogo ya North Horr aliyeripotiwa kupotea siku 3 zilizopita amepatikana akiwa ameaga dunia.

Konstabo Abdiaziz Mohammed Aden aliripotiwa kutoweka siku ya Jumatatu wiki hii.

Mwili wake uliokuwa umeanza kuoza ulipatikana na wafugaji eneo la Araftis, lokesesheni ya Sabare wadi ya Dukana ukiwa unaninginia kwa mti.

Wafugaji hao walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Dukana ambao walitembelea eneo la kisa kwenye barabara ya Sabare-Buluk.

Ripoti ya polisi imedhibitisha kuwa mwili wa mwendake ulipatikana ukiwa unaning’inia kwa mti ukiwa umefungwa kwa kamba kuashiria huenda alijitia kitanzi.

Aidha, begi ilipatikana karibu na mwili huo huku nguo zimetapakaa kwenye barabara.

Mwili umesafirishwa hadi kituo cha polisi cha Dukana.

Subscribe to eNewsletter