Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Adho Isacko
Wakaazi wa eneo la Karare wamekosa kuafikiana na shirika la kutathmini athari za ujenzi kwa mazingira, maafisa wa shirika la wanyamapori KWS pamoja na jeshi la KDF kwenye mkutano uliofanywa hiyo jana ili kutathmini athari za ujenzi wa kambi ya jeshi katika eneo hilo.
Wakaazi hao wanadai kuwa wengi wao hawakuwa wameelewa lengo la mkutano huo na hivyo kuwa vigumu kwao kutoa maoni yao.
Waliojadili wamedai kuwa pahala hapo ni muhimu kwa sababu za kitamaduni.
Kwa upande wake mkaazi mwenginemichael leala, amesema kuwa, wamewaeleza wakuu hao kuwapa muda ufaao ili waweze kujadili na kuleta suluhisho kwa changamoto wanazopata kabla ya kuziwasilisha kwao.
Jonah lengelen amesema kuwa tangu kambi hiyo kutangazwa kuwekwa wakaazi wa karare wamepata changamoto nyingi sana ya hivi punde zaidi ikiwa ni idadi ya ndovu ambao wamekuwa wakionekana kwenye vijiji kila wakati.
Akiongoza mkutano huo naibu kamishna wa marsabit ya kati patrick murira alikuwa na haya ya kusema.