Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Jillo Dida
Shehena ya bangi iliyokamatwa katika barabara kuu ya Moyale hadi Isiolo na katika kaunti ya Marsabit imeteketezwa mjini Marsabit.
Hakimu mkaazi wa mahakama ya Marsabit Tom Mbayaki Wafula aliongoza zoezi hilo la kuteketeza bangi hiyo yenye dhamana isiojulikana.
Kati ya mwaka 2017 na mwaka 2020 takriban kesi 117 zinazohusiana na bangi zimewasilishwa mbele ya mahakama ya mjini Marsabit.
Akizugumza na wanahabari katika halfa hiyo siku ya alhamisi katika kituo kuu cha polisi cha Marsabit, Wafula alibaini kuwa kesi 22 kati ya kesi 117 ziliondolewa na upande wa mashtaka.
Aidha shughuli hiyo ya uketeketezaji ilitekelezwa kwa ushirikiono na polisi pamoja na maafisa wa mahakana ya Marsabit.
Hata hivyoamewataka wakazi kuacha kujihusisha na biashara ya zao hilo,na badala yake wafanye biashara halali zitakazo wasaidia kuingiza kipato bila kusumbuliwa na serikali.
Amedokeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watuhumiwa wote na kuitaka jamii kutoa ushirikiano kudhibiti dawa hizo ambazo zimekuwa na madhara kwa taifa.
Wafula ameongeza kuwa shughuli zote za mahakama zikiwemo za mahakama tamba zimesitishwa kwa muda katika kaunti ya Marsabit kuambatana na maagizo ya wizara ya afya kuzuia msambao wa virusi vya corona.