Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Adano Sharawe
Kwa mara ya kwanza waumini wa kiislamu jimboni marsabit hawatahudhuria swala kama kawaida katika misikiti baada ya kufungwa kuzuia maambukizi ya corona.
Katika taarifa, mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri SUPKEM jimboni Jarso Jllo Fallana amesema baada ya mashauriano baina ya viongozi wa misikiti, wameamua kufunga misikiti kwa muda ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.
Wakizungumza baada ya kukutana na kamishna wa kaunti hii evans achoki afisini mwake, viongozi hao wametaka waumini kuendelea na swala kama kawaida Hapo manjumbani mwao kuzuia mikusanyiko ya makundi ya watu wengi.
Hata hivyo viongozi hao wamesikitikia hatua ya baadhi ya watu kupuuza amri ya serikali ya kujikinga.
Pia wametoa wito kwa wananchi wote kuchukulia kwa uzito muongozo wa serikali kuhusu maambukizi hayo ili kuzuia ueneaji wa virusi hivyo.
Wengine waliokuwepo ni mwenyekiti wa maimamu sheikh mohamed galgallo, sheikh mkuu wa msikiti wa jamia sheikh mohamednorr kuli kati ya wengine.
Kwa mujibu wa SUPKEM Kuna jumla ya takriban misikiti 20 hapa mjini marsabit.
Haya yanajiri siku moja to baada ya mabaraza ya kiislamu nchini SUPKEM na KEMNAC kuwaomba waislamu nchini kuifunga miskiti kwa siku 14 kama ilivyoangizwa na serikali na badala yake kuwataka waislam kutekeleza ibada zao za swala majumbani ili kudhibithi maambukizi ya virusi vya corona.
Hadi sasa watu 16 wameambukizwa ugonjwa wa covid-19 nchini kenya na hivyo kuna hofu kuwa homa hiyo hatari itaenea kwa kasi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.
Kwa upande wake kamishna achoki amepongeza viongozi hao wa misikiti kwa hatua hiyo inayoambatana na muongozo wa serikali kuzuia mikusanyiko ya watu wengi.
Achoki amesisitiza kwamba serikali imeweka mikakati yote hitajika katika kuzuia janga hili kuenea.
Ametangaza marufuku kwa shughuli zote zinazohusisha mahudhurio ya watu wengi kama vile harambee, harusi, matanga na burudani wa aina yoyote.
Amewataka machifu na manaibu wao kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kikamilifu
Kando na viongozi hao wa misikiti, achoki amebaini kuwa amekutana na wenye vilabu na maeneo ya burudani ambao wamekubali kufuata muongozo wa serikali na kusitisha shughuli kwa muda wa siku 30.