Highlights

Watu watatu wakamatwa kwa wizi wa mifugo Loiyangalani

Na Joseph Muchai

Watu watatu wamekamatwa na maafisa wa polisi wakihusishwa na wizi wa mifugo katika eneo la Loiyangalani kaunti ya Marsabit.

Hii ni kutokana na operesheni ambayo imekuwa ikiendelea katika eneo hilo ya kurejesha mifugo waliobiwa mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na Shajara OCPD wa Loiyangalani Nicolas Mutua, amethibitisha kuwa washukiwa hao watafikishwa mahakamani siku ya hapo kesho Alhamisi.

Aidha Mutua amedokeza kwamba kwa sasa wameweza kupata zaidi ya mifugo 470 kwa ushirikiano na wazee kutoka jamii zote husika.

Wakati uo huo ametoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na asasi za usalama ili kuhakikisha kuwa oparesheni hiyo inafanikiwa na visa vya wizi wa mifugo vinadhibitiwa kikamilifu

Post Comment