Highlights

Vijana Marsabit watoa hisia mseto kuhusu mtaji wa mradi wa Nyota.

Na Nyabande Orwa

Vijana katika kaunti ya Marsabit wametoa maoni tofauti kuhusu mradi wa NYOTA unaotekelezwa na serikali ya kitaifa kwa lengo la kuwapa mtaji wa kuanzisha na kuendeleza biashara.

Baadhi ya vijana waliozungumza na kituo hiki wamesema mchakato wa kuwachagua wanufaika haukuwa wa haki. Wanasema kuna vijana walioteuliwa lakini majina yao hayakuonekana katika orodha ya waliopata fedha za mradi huo. Kutokana na hilo, vijana hao wameikosoa serikali kwa kile walichokitaja kama kushindwa kutimiza ahadi ya kuinua vijana walioko chini kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Hata hivyo, kuna vijana wengine wanaosema mchakato huo ulifuata utaratibu uliowekwa, na kwamba waliopata nafasi walibahatika. Wanasema fedha za mradi wa NYOTA zitawasaidia kuimarisha biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Joseph Leruk ni mwakilishi wadi wa Karare anaeunga mkono mradi wa Nyota akisema ni afueni kwa vijana wanaohangaika na umasikini.

Katika hafla iliyofanyika Achers Post kaunti ya Samburu, vijana Elfu Moja Mia Tano Na Tatu kutoka Marsabit walinufaika na mradi huo, ambapo kila mmoja alipokea shilingi elfu ishirini na tano za awamu ya kwanza. Wanatarajiwa kupokea shilingi Elfu Ishirini Na Tano nyingine baada ya majuma kadhaa, kulingana na Kamishna wa Kaunti ya Marsabit, James Kamau.

Post Comment