Wito wa kuimarisha elimu ya mtoto wa kike watolewa, Marsabit
Na JB Nateleng
Licha ya kaunti ya Marsabit kukaribia kurekodi usawa wa kijinsia miongoni mwa watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa KCSE 2025, wanaharakati pamoja na wadau wengine wametakiwa kuongeza juhudi za kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike jimboni.
Takwimu zinaonyesha kuwa wasichana walikuwa asilimia 49.15 huku wavulana wakiwa asilimia 50.85 hali inayodhihirisha hatua kubwa kuelekea usawa wa kijinsia katika elimu.
Kulingana na Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Marsabit Women Advocacy Development Organization (MWADO) Nuria Gollo, bado ipo haja ya kuwekeza juhudi zaidi ili kuhakikisha kwamba jamii ya Marsabit inakumbatia elimu ya mtoto wa kike na kuacha mila potovu inayodunisha na kudharau haki za mtoto wa kike kupata elimu.
Nuria amepuzilia mbali madai kuwa mtoto wa kiume ametelekezwa na jamii, akisema kwamba haki ya mtoto wa kiume inalindwa na anawezeshwa kwa usawa na mtoto kike.
Nuria kadhalika ameongeza kuwa ushirikiano kati ya wazazi, Idara ya elimu pamoja na wanaharakati utahakikisha kwamba watoto wao wanahudhuria masomo.



Post Comment