Washukiwa wawili wa mauaji wapatikana na hatia, marsabit
Washukiwa wawili wa mauaji wamepatikana na hatia katika mahakama kuu ya Marsabit.
Wawili hao Bonaya Abkula na Halakhu Dida wamepatikana na kosa la kumpiga na kumsababishia kifo marehemu Guyo Jaldesa mnamo tarehe 13 mwezi Septemba mwaka 2024 katika lokesheni ya Manyatta Jillo kaunti ndogo ya Marsabit Central.
Mshukiwa wa kwanza anasemekana kumvamia marehemu kwa fimbo huku mshukiwa wa pili akimpiga kwa mikono na mateke walipokuwa wakidai shilingi 100 alizodaiwa kuchukua.
Marehemu alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.
Akitoa uamuzi huo leo Alhamisi, Jaji wa mahakama kuu ya Marsabit Francis Rayola amesema kuwa upande wa mashtaka, uliowasilisha mashahidi wanane, ulithibitisha kuwa wawili hao walihusika katika kifo cha marehemu Guyo Jaldesa.
Jaji Rayola ameipa idara ya probesheni siku 21, kuwasilisha ripoti kuhusu maisha ya wawili hao kabla ya uamuzi wa hukumu kutolewa.


Post Comment