Highlights

Mtoto wa chini ya siku 3 apatikana ametupwa kando ya barabara, Marsabit Central

NA Sabalua Moses

Mtoto wa chini ya siku tatu amepatikana akiwa ametupwa kando ya barabara katika eneo la Riverside kaunti ndogo ya Marsabit Central.

Akithibitisha kisa hicho cha Jumanne jioni, OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago, amesema kuwa msamaria mwema alimpata mtoto huyo wa kike akiwa amefungwa na mavazi na kupiga ripoti katika kituo cha polisi.

Ripoti hiyo pia iliwasilishwa katika idara ya watoto.

Mtoto huyo yuko katika hali nzuri na anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Marsabit, kabla ya kupelekwa katika makao salama.

OCPD Gachago ametoa wito kwa umma kutoa ripoti yoyote kuhusu mama ya mtoto huyo huku pia mzazi huyo akiombwa kujiwasilisha kituoni.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment