Highlights

Wananchi walio karibu na Ziwa Turkana watakiwa kuchukua tahadhari msimu huu wa mvua.

Na JB Nateleng

Wakaazi wanaoishi kando ya Ziwa Turkana kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwa waangalifu zaidi msimu huu wa mvua ili kujikinga dhidi ya mashambulizi ya mamba.

Akizungumza na Shajara mwenyekiti wa Kitengo cha Usimamizi wa Ufuo wa Bahari (BMU) cha Loiyangalani, Martin Losunyen, amesema ni muhimu kwa wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka maeneo yanayojulikana kuwa mazalia ya mamba.

Losunyen pia amewatahadharisha wavuvi wanaoendelea na shughuli za uvuvi katika Ziwa Turkana kuhakikisha wanatumia vifaa vinavyofaa na salama ili kupunguza hatari ya kukumbana na mamba.

Aidha, amewashauri wanafunzi pamoja na wageni wanaotembelea Ziwa Turkana kufuata maelekezo ya wanachama wa BMU au maafisa wa uvuvi kuhusu maeneo salama ya kutembelea ili kuepuka hatari ya kushambuliwa na mamba.

3 comments

comments user
Nicholas nyangura koriye

The fishermen’s are in dangers during this seasons of rain,no fishing by foot’s because the lake is increased and attack’s from water animals.displacement and alot of mosquitoes 🦟 this time round they need government help

comments user
Nicholas nyangura koriye

Both fishermen’s and pastoralist are in dangers,need urgent help from the government and non government 🙏
From Nicholas nyangura Illolo beach management unite chairman

comments user
Üsküdar Duvar İçi Su Kaçağı Tespiti

Radio Jangwani 106.3FM ni pride ya Marsabit! Keep informing, educating, and entertaining us!

Post Comment