Highlights

ODPP Marsabit yafundisha mahabusu njia mbadala za kesi na makubaliano ya kukiri kosa

Na Nyabande Orwa

Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma  katika kaunti ya Marsabit , ikiongozwa na mkuu wa kaunti Joseph Mburugu, pamoja na mawakili wa mashtaka Shadrach Nderitu na Omar Weteka, wamezuru gereza la Marsabit.

Katika ziara hiyo ya siku ya siku ya Jumatano, maafisa hao waliwapa mahabusu elimu kuhusu sera za afisi hiyo zinazohusu njia mbadala za kushughulikia baadhi ya kesi bila kufika mahakamani, inayojulikana kama diversion, pamoja na utaratibu wa makubaliano ya kukiri kosa kati ya mshukiwa na upande wa mashtaka, unaojulikana kama plea bargain.

Kwa mujibu wa Joseph, kwa mahabusu waliofungwa na waliowekwa rumande mchakato wa kukiri kosa kunawasaidia kutosalia gerezani kwa muda mrefu.

Aidha, kama ishara ya kuonyesha nia njema, timu hiyo ilitoa msaada wa baadhi ya mahitaji muhimu kwa wafungwa walioko katika gereza hilo.

Post Comment