Highlights

Wananchi saku wahimizwa kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura

NA Caroline Waforo

Wananchi katika eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wamehimizwa kujitokeza kwa wingi ili kujisajili kama wapiga kura katika zoezi linaloendelea kote nchini.

Kulingana na afisa anayesimamia tume ya uchaguzi na mipaka IEBC tawi la Saku, Wilson Kidenye, kwa sasa idadi ya wanaojisajili ipo chini.

Hadi kufikia sasa ni watu 88 pekee ambao wamejisajili kama wapiga kura wapya, huku wapiga kura 68 wakihamisha kura zao kutoka maeneo mengine ya taifa hadi eneobunge la Saku.

Haya ni huku tume ya IEBC ikipania kufanya zoezi la usajili wa wapiga kura kwa wingi hivi karibuni.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment