Joto na ukavu kuendelea kushuhudiwa jimboni Marsabit- Idara ya hali ya anga yadokeza
NA Caroline Waforo
Vipindi vya jua mchana vitaendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Marsabit huku mawingu yakitarajiwa katika sehemu nyingi za jimbo nyakati za usiku.
Haya ni kulingana na ripoti ya utabiri wa hali ya hewa katika siku 7 zijazo kuanzia leo tarehe 20 hadi tarehe 26.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa joto la mchana jimboni, linatarajiwa kufikia nyuzi joto 30 huku baadhi ya maeneo katika eneobunge la Saku na Mt Kulal likitarajiwa kushuhudia kijibaridi cha asubuhi.
Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa kaunti ya Marsabit John Nguyo kaunti ya Marsabit haitashuhudia vipindi vya mvua.
Aidha eneo la Loiyangalani linatarajiwa kushuhudia upepo mkali huku maeneo mengine jimboni yakipata upepo mwepesi.



Post Comment