Highlights

Bwawa la Bakuli kutosheleza maji kwa kipindi cha miwezi miwili tu-MARWASCO yasema

NA Caroline Waforo

Huenda hali ya uhaba wa maji ikawa mbaya zaidi katika kaunti ya Marsabit, kutokana na athari za kiangazi kinachoshuhudia jimboni kufuatia kufeli kwa mvua za msimu wa mwezi October, November na December mwaka jana.

Kulingana na John Halkano Guyo ambaye ni afisa katika kampuni ya kutoa huduma za maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO, bwawa la Bakuli linaweza kutosheleza mahitaji ya maji kwa kipindi cha miezi miwili tu ijayo.

Amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo inalazimika kuwapa wananchi maji kwa vipimo ili kuhakikisha kuna usawa na utoshelevu wa maji yaliyopo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment