Highlights

KUPPET Marsabit yashutumu baraza la mitihani KNEC kwa kutowawajibisha wezi wa mitihani.

Na Samuel Kosgei

KATIBU wa chama cha kutetea maslahi ya walimu KUPPET tawi la Marsabit Sarr Galgalo ameikosoa baraza la mtihani nchini KNEC kwa madai ya kuruhusu udanganyifu katika matokeo ya mitihani ya kitaifa KCSE.

Sarr akizungumza na Radio Jangwani amesema kuwa matokeo ambayo wanafunzi haswa katika mkoa wa kaskazini mwa nchi ni ya urongo na hayaoneshi picha kamili ya uwezo wa wanafunzi.

Ametolea mfano baadhi ya wanafunzi waliojisajili kufanya mtihani wa KCSE katika shule za North Eastern ilhali wanasomea shule za kaunti nyingine na matokeo yao yanafahamika vyema.

Anasema wanafunzi ambao wamekuwa wakifeli mitihani katika kidato cha kwanza hadi tatu wanaibukia kupata alama za juu katika mtihani wa KCSE suala analodai lina udanganyifu mkubwa.

Ameonya wazazi dhidi ya kukubali kulipia wizi wa mitihani akisema itaadhiri maisha ya wanao.

Mwalimu Sarr anasema wizi wa mitihani unasababisha wanafunzi waliopata alama za juu kushindwa kumaliza kozi ngumu kwani sio alama zao za kweli na hawana uwezo wa kumudu kozi walizoitwa hatua inayochangia wao kuacha masomo.

Post Comment