Highlights

Walengwa wa HSNP Marsabit kupokea malipo ya miezi mitatu mwezi huu wa January.

Na Samuel Kosgei

SERIKALI kupitia mamlaka ya kitaifa ya kukabili ukame NDMA imeanza kusambaza pesa za kusaidia familia zisiojiweza na zinazoishi katika hali ya umaskini jimboni Marsabit kupitia programu ya HSNP.

Kupitia mkurugenzi wa programu hiyo ya HSNP Jonah Samana, serikali itasambaza pesa za miezi 3 zinazolenga boma 20,453 katika maeneo bunge manne ya Marsabit.

Familia 5,057 zitafaidi eneobunge la Laisamis, Saku 4,225, Moyale 6,037 na North Horr 5,070. Familia zilizotajwa zitapokea shilingi elfu 8,100.

Kulingana na Samana wafaidi wa mradi huo wameombwa kuzidi kusubiri deni la miezi iliyosalia kwani italipwa pindi bunge litakapoidhinisha bajeti ya ziada.

Hata hivyo amesema kuwa hivi karibuni mamlaka hiyo itafanya tena usajili upya wa walengwa wengine kutokana na mradi huo HSNP kufikia kikomo baada ya miaka mitano.

Post Comment